Mwaandishi wetu
Jeshi la Polisi nchini limewaomba
viongozi wa dini kukemea baadhi ya maneno yanayotamkwa na wanasiasa badala ya
kukaa kimya.
Ombi hilo limetolewa Inspekta wa Polisi Simon Sirro wakati alipokuwa anaongea na viongozi wa dini visiwani
Zanzibar, kuhusuiana na suala la amani, katika kipindi chote cha uchaguzi
ambapo amesema viongozi wa dini ni moja ya wadau wa amani nchini.
"Niwaombe sana kwasababu
mnasikia baadhi ya maneno yanayotamkwa na baadhi ya wanasiasa lakini mmekaa
kimya hamsemi, mmekaa kimya hamkosoi, mmekaa kimya mekuwa woga niwaombe sana ni
muda sasa kuona kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tulikemee", - alisema IGP
.Sirro.
Sirro amesema kuwa baadhi ya viongozi wa dini
hawako kwa ajili ya kusaidia watanzania badala yake wapo kwasababu ya tama
waliyonayo ya kutaka madaraka .na amewaonya viongozi wote wa dini wanaojihusisha
na uhalifu kuwa atawachukilia hatua bila kujali nafasi yao katika jamii kwani
ukikiuka sheria lazima uadhibiwe kwa mujibu wa sharia.
"Padri ukishajiingiza kwenye
uhalifu mimi ntakushughulikia kama uhalifu mwingine, Padri ukishakuwa mbakaji
ntakugonga kama mbakaji mwingine, Shehe/Padri ukijiingiza kwenye ugaidi
ntakushughulikia kama gaidi hiyo kwasababua heshima ina ukubwa zaidi kuliko mtu
binafsi" alisema IGP Sirro
0 Comments