Mwanja Ibadi
Lindi
ALIYEKUWA Mgombea ubunge jimbo la Lindi Manispaa kupitia
ccm Mohamedi Mtali amesema kuwa amekubali matokeo ya uteuzi wa
mgombea Mbunge jimbo hilo ulifanywa na
vikao vya juu vya chama chake na kueleza
kuwa atamuunga mkono mgombea aliyependekezwa na
vikao vya juu
vya chama hicho
Haya ameyaeleza leo jumamosi tarehe
22 august wakati alipokuwa anazungumza
na waandishi wa habari.
Utali alisema mchakato wa kuwatafuta
wagombea ubunge na udiwani kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) umekamilika tarehe 20 augost 2020 kwa Halmashauri
kuu ya Taifa Ccm kuteua wagombea katika
majimbo yote nchini.
Alisema kuwa kwa
matokeo hayo , wanachama wote ,
viongozi na wapenzi wa chama mapinduzi kuacha tofauti zao
zilizoibuka wakati wa
mchakato wa kumtafuta
mgombea badala yake washikamane
pamoja na kuhakikisha
chama chao kinapata ushindi
katika nafsi za udiwani, ubunge, na
urais.
Utali alisema ni wakati wa viongozi
wa chama cha mapinduzi
mkoa wa Lindi katika
ngazi za matawi , kata
wilaya, kuhakikisha wanafanya juhudi
kubwa za kutibu majeraha
yaliyotokana na uteuzi wa
wagombea wa ubunge na udiwani ,
ili wanachama na wapenzi kuwa kitu kimoja kuleta ushindi.
0 Comments