Mwaandishi wetu
Serikali imewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri na
wakuu wa wilaya hapa nchini kutoa majengo kwa ajili ya matumizi ya
ofisi za taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru pale ambapo taasisi
hiyo haina majengo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa
nchi utawala bora George Mkuchika wakati akizindua jengo la taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma na kusisitiza kuwa, ni
haki kwa Takukuru kutumia majengo ya Serikali pale inapokosa ofisi kwa
ajili ya kutoa huduma kwa wananchi
Alisema, kuna majengo yasiozidi
thelathini kati ya mahitaji ya majengo zaidi ya mia moja nchini ,kwa hiyo
pale taasisi hiyo inapokosa ofisi ni wajibu wa viongozi wa eneo husika kutoa
majengo ya serikali yaliyopo ili yatumiwe na Takukuru.
“nisije kusikia eti wilaya fulani
takukuru imekosa majengo ya kufanyia kazi, jambo hilo sitokubaliana nalo hata
kidogo,ni wajibu wa viongozi kutafuta na kutoa majengo kwa takukuru pale ambapo
Serikali haijajenga majengo ya Takukuru”alisema Mkuchika
.
Waziri Mkuchika mapambano
dhidi ya rushwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano imesaidia
kuharakisha maendeleo na kukua kwa uchumi ambapo ripoti ya Benki ya Dunia
ya Septemba mwaka jana, imeitaja Tanzania imeongoza kupunguza umaskini
miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Alisema, ripoti nyingine ya Benki ya
Dunia inayoitwa(Human Capital the Real Wealth of Nations ya Julai 2019
ilionesha umaskini nchi I Tanzania umepungua kutoka asilimia 34.4 hadi kufikia
asilimia 26.8.
2018/2019 zimeendelea kuonekana kupitia
taarifa za utafiti wa kupima hali ya rushwa Duniani unaofanywa na wadau
mbalimbali wa mapambano dhidi ya rushwa na utawala bora.
Mkuchika alisema, kufunguliwa kwa
ofisi ya Takukuru wilayani Namtumbo ni ushahidi tosha na namna gani Serikali ya
awamu ya tano ilivyodhamiria kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa
kuijengea uwezo zaidi kiutendaji taasisi hiyo
Ameitaka Takukuru kuhakikisha
wananchi wanapata haki wanazostahili popote wanapokwenda kupata huduma na pale
wanaponyang’anywa na mtu au taasisi yoyote kwa njia za rushwa.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina
Mndeme, ameipongeza Takukuru kwa kazi nzuri inayofanya katika kuzuia na
kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa hapa nchini.
Alisema, jengo hilo ni muhimu sana
katika kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa Takukuru watakaopangiwa
kufanya kazi katika wilaya ya Namtumbo na litawarahisishia watoa taarifa pamoja
na mashahidi watakaoletwa katika operesheni mbalimbali kuwa na uhuru na usiri
mkubwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Sabina Seja
alisema,hadi kufikia mwezi julai mwaka huu Takukuru imejenga jumla ya ofisi za
mikoa 28 na ofisi katika wilaya 117,lakini kati ya ofisi hizo majengo
yanayomilikiwa na Takukuru ni 22 kwa ngazi ya mikoa na majengo 22 katika
wilaya.
0 Comments