WAISLAMU LINDI WAASWA KUFUTILIA MWENENDO WA WATOTO


Mwandishi wetu

 Waislamu  mkoa Lindi wametakiwa  kutoa malezi bora kwa watoto  na  kuwapa elimu  ili kuwajenga  na kuwaandaa kuwa  raia wema  wa  badaye.

 Wito huyo  umetolewa  na shekhe mkuu  mkoa  wa Lindi  Mohamedi Mshangani  wakati  alipokuwa anazungumza  na viongozi  wa Dini ,watu  maharufu  vijana  na makundi  ya  akina mama kwenye  semina ya siku tatu ya masuala ya  mbalimbali ikiwemo uzazi wa mpango,na  afya  iliyoandaliwa  na  baraza la  waislamun Tanzania Bakwata

Mshangani  alisema kuwa  ni jambo jema kwa  wazazi kutoa malenzi  bora  kwa  watoto  sambamba  na  kuwapigania  wapate  elimu  ili kuwaandaa kuwa  viongozi na  raia wema wa baadaye.

"Mtoto mwema anatengezwa na  wazazi, futilieni mwenendo  na muwachunguze wa watoto wenu" ,,, alisema shekhe Mshangani 

Aidha  kwenye  mafunzo hayo washiriki  walijifunza  mambo  mbalimbali  ikiwemo ya  madhara  ya  mimba  za utotoni,faida  ya  uzazi wa mpango.



Post a Comment

0 Comments