LINDI KUMEKUCHA MGOMBEA UBUNGE ACT AWASHA MOTO
Mwandishi wetu
Mgombea ubunge katika jimbo la Lindi kupitia Chama cha Alliance
for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Isihaka Mchinjita amehaidi kuanza
kushughulikia sekta ya elimu, uvuvi na kilimo iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa
jimbo hilo.
Mchinjita ametoa ahadi hiyo leo katika mtaa wa Mnazimoja, manispaa
ya Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ubunge jimbo la Lindi.
Mchinjita ambae ni mwalimu alisema anatambua kwamba jimbo hilo
linachangamoto nyingi. Hatahivyo akichaguliwa na kuwa mbunge ataanza
kushughulikia changamoto zilizopo kwenye sekta za kilimo, uvuvi na elimu.
Alisema kuwa kwenye
sekta ya elimu, jimbo la linahuaba wa
shule za msingi na sekondari. Hali inayotokana na waliokuwa wabunge wajimbo
hilo kutotambua umuhimu wa elimu kwa maisha na maendeleo ya wananchi.
Alisema jimbo hilo linamitaa takribani 137. Hata hivyo lina shule
za msingi 133. Hali inayosababisha baadhi ya watoto kutembea umbali mrefu
kwenda ziliko shule. Huku akiongeza kusema kwamba jimbo hilo lina shule za
sekondari kumi tu.
" Hata shule ya sekondari ya Lindi ambayo baadhi ya majengo
yake yaliungua moto haijakarabatiwa licha ya michango iliyofanyika
nakufanikisha kukusanya takribani shilingi milioni mia nane. Kuwanyima watu
elimu nisawa na kuuwa maarifa ya kizazi husika," alisema Mchinjita.
Mchinjita alisema kutokamilika mradi wa mtambo wa kuchakata gesi
asilia( NLG) ambao unatarajiwa kujengwa katika manispaa ya Lindi. Kwani mtambo
huo ungeweza kutoa ajira takribani 5,000 ambazo zingesababisha mzunguko mkubwa
wa fedha kwa wananchi wa jimbo hilo na mkoa wa Lindi.
Alibainisha kwamba mji wa Lindi hauna harakati za kiuchumi zenye
tija na umedorora. Kwani shughuli zimekuwa ngumu kutokana na kutokuwa na
viwanda ambavyo wafanyakazi na vibarua wa viwanda wangeweza kununua bidhaa za
madukani, vyakula kungekuwa na wageni wengi ambao wangelala kwenye nyumba za
kulala wageni. Hata hivyo kwasasa biashara zote hizo ni ngumu.
Alisema kuachanana mradi wa gesi kuna hasara kwa wananchi wa mikoa
hiyo ambao waliamini ndani ya miaka mitano baada ya ugunduzi huo wangekuwa na
uchumi nzuri ambao ungetokana na gesi hiyo ambayo alisema ugunduzi wake
unaashiria kuwepo mafuta.
0 Comments