Mwandishi wetu

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar  kwa tiketi ya Chama cha Maoinfuzi CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi endapo atachaguliwa kuwa Urais wa Zanzibar  atahakikisha Serikali ambayo ataingoza itakuwa serikali inayosikiliza wasomi na wananchi.

Hayo ameyasema Jana Tunguu kusini Unguja wakati akihutubia vijana kwenye mhahalo wa vijana wa CCM uliomdaliwa na Idara ya vyuo na vyuo  vikuu ambalo lengo la mdahalo huo kujadili mambo mbalimbali kwa mustakabali wa chama cha Maoinduzi CCM.

Dk Mwinyi alisema kwamba endapo harakati zitakamilika na kuwa Rais wa Zanzibar  atahakikisha kuwa serikali bayo ataiunda inawasikiliza kindi la wasomi na wananchi kwa ujumla.

  Dk Mwinyi aliwatoa hofu  vijana wa chama cha Mapinduzi CCM kwamba Serikali inayokuja itahakiksha inakwenda kuendeleza yale yote yaliyofanywa na awamu iliyopita katika kutatua changamoto zinazokabili watu wenye ulemavu.