NA BASHIRU KAUCHUMBE, RUANGWA
Uamuzi wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wa kupeleka Ofisi za Ardhi kila Mkoa badala ya kuwa na Ofisi za Kanda, umeonesha mafanikio makubwa ya kurahisisha upatikanaji wa hati za kumiliki ardhi kwa haraka.
Hali hiyo imedhiirishwa kwa wakazi wa wilaya ya Ruangwa wapatao 69 ambao wamepatiwa hati za kumiliki Ardhi katika Hafla fupi ya kukabidhiwa hati iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.
Akikabidhi hati hizo kwa wanachi hao Msajili wa Hati wa Mkoa wa Lindi Bwana Godfrey Faramagoa amesema dhima ya kufanya hivyo ni kurasimisha na kuhamsisha wananchi ambao wanaviwanja ambavyo wamevipata kwa kufuata utaratibu wa kisheria kujenga utamaduni wa kupatiwa Hati za kumiliki Ardhi.
Amezitaja faida za kuwa na hati za kumiliki hati za Ardhi ni pamoja na kuongeza thamani ya Ardhi/Kiwanja na Mashamba,Hati inaweza kutumika kwa dhamana kwa mwananchi pindi wanaposhikiliwa na jeshi la Polisi au kufikishwa mahakamani ,pamoja na kutumika kama dhamana ya Mikopo katika taasisi za Kifedha au Mikopo ya kilimo .
Kwa upande wake Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Bwana Peter Hanjay amesema kuwa upatikanaji wa Hati za kumiliki Ardhi itakuwa rahisi kutokana na Wizara kusogeza huduma karibu katika ngazi ya Mikoa tofauti na awali Hati zilikuwa zinatolewa na Ofisi za Kanda kitu ambacho kilichangia wananchi wengi kushindwa kuzifuata hati hizo kwa kushindwa kumudu gharama za usafiri na malazi ,Lakini kwa sasa Mwananchi akishakamilisha Taratibu zote anapatiwa hati yale ndani ya siku saba
Hanjay amewasisitiza wakazi wa Ruangwa kuchangamkia fursa hii kwa kuanza michakato ya kupata hati za Kuliliki Ardhi ,amesema Ofisi yake ipo wazi na ipo tayari kutoa huduma hizo.
Bi Maimuna Pendeka ni Miomngoni mwa Wananchi waliopata hati hizo ,Ameishukuru wizara kwa kufungua Ofisi ngazi Ya Mkoa kwani yeye alishakamilisha mchakato wa kupata Hati Toka mwaka 2016 lakini alishindwa kuifuata Mtwara Mtwara kutokana na kushindwa gharama za Nauli na pesa za kujikimu.Pia amesema kuwa Hati hizo zitamsadia kupata Mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuendeleza shughuli zake za kinishara.
Akijibu hoja za wananchi katika Hafla hiyo fupi kuhusu makazi yasiyo rasimi ambayo yamejengwa pasipo kuzingatia mipango miji,Afisa Mipango miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bwaba Isihaka Panja amewashauri wananachi wanaohitaji mpango miji katika eneo lao au kurasiisha mashamba ni wakati wao sasa kujiunganisha pamoja kwa kushirikiana na Mamlaka za Vijiji au Mitaa kwa kushirikiana na Idara ya Ardhi ili kuweza kuandaa mchakato wa kurasimisha maeneo hayo.
Jumla ya Hati 193 zimetolewa kwa Mkoa wa Lindi mbapo Wilaya Liwale zimetolewa Hati 40,Nachingwea Hati 24 na Ruangwa Hati 69.
0 Comments