Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Tanzania (JKT) Brigedia Jenerali Charles
Mbuge kupitia muwakilishi wake Kanali Philipo Mahende, amewataka
wahitimu 987 wa mafunzo ya awali ya kijeshi na uzalishaji mali kwa
mujibu wa sheria, uparesheni uchumi wa kati 2020 kikosi cha 843KJ
Nachingwea Lindi kufanya kazi kwa vitendo ili kujikwamua na umasikini na
kutazama fursa zitakazoweza kuwasaidia na sio kuilalamikia serikali
muda wote.